Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, September 28, 2009

NANI KAMA MAMA-INAENDELEA

 Je huyu mgonjwa ameenda wapi,na kipi kimemsibu, haya na mengine mengi yalikuwa maswali wakijiuliza madakitari , na ilibidi wamuite yule nesi ili aeleze kilichotokea. Yeye alijitetea kuwa alitoka kidogo kwenda kuchukua dawa na dripi kwasababu iliyokuwepo ilikuwa inaanza kuisha, aliporudi akakuta mlango upo wazi, na alipoingia ndani akakuta mgonjwa kachomoa ile mipira yote mwilini mwake na ametoweka humo ndani.

`Jeulijaribu kutafuta vyumba vingine' walimuuliza
`Hapana nilipoona hivi nilikimbilia kuwafahamisha..' alisema huku akitetemeka

Madakitari wakaamurisha msako uanze mara moja,na mkuu wa ulinzi akapewa taarifa. Je walimpata huyo mgonjwa? Nitaendelea kuielezea hili tukio,lakini kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu, vitendea kazi, sehemu ya kazi nk ninashindwa kuiendeleza. Tuombe mungu kama nitapata sehemu ya kuweza kuifanya hii kazi vizuri.
From miram3

2 comments :

Anonymous said...

M3 PLZ TUNAOMBA SN UMALIZIE HII STORY NI NZURI SN NA INAFUNDISHA,UNA STORY NZURI SN UNANIFANYA HATA NISHINDWE KUSOMA,YN NI LAZIMA KILA SIKU NIPITIE HAPA NDO NIENDELEE NA KAZI ZANGU NYINGINE...NTAFURAH SN KM UTAIENDELEZA STORY HII

emu-three said...

Nimefurhi kunikumbushi kumalizia hiki kisa, na nitajitahidi kufanya hivyo, tuombe mungu hawa Tanesco watujali, kwani kwetu usiku ni giza, sijui mgawo gani wa usiku, na hapa ofisini, mmmmh, nikujiiba...nitajitahidi niendelee nayo,usijali sana