Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeMonday, September 14, 2009

MTOA RIZIKI NI MUNGU

Ilikuwa jumatatu ya kipekee (blue monday), nikiwa nimefika asubuhi mapema kama kawaida yangu, nikakuta ofisi hazijafunguliwa ,baadae kitambo alifika bosi wa kampuni na kufungua mlango. Aliniangalia kwa jicho ambalo kwangu mimi niliona ni la chuki au kuogopa au vinginevyo, kwa mtizimo wa haraka alikuwa hayupo katika hali ya kawaida(good mood). `Hii hutokea kwa kila mtu, siku zote sio sawa!' nilijisema moyoni. Niliingia ndani huku moyo ukinidunda, sikuelewa kwanini moyo ulikuwa ukinidunda hivyoi,nikahisi kuna kitu kinakuja.

Nilifika mezani nikiwa na hamasa ya kusoma habari za siku mbili zilizopita na kugundua kuwa mitandao inashida kupatikana. Baadaye walifika wafanyakazi wengine, na mara yule bosi wakampuni akaja kwenye kitengo chetu na kumuita kiranja wa kitengo, alimuagiza achukue faili fulani ndani ya kabati,ilikuwa sauti ya chini kwahiyo sikusikia ni faili gani. Moyo ulizidi mapigo.

Mara yule baosi alirudi tena kwenye kitengo chetu na mara hii aliniita mimi. Sio kawaida yake kuniita mimi,kama ni kazi hutoa kwa kupitia kiranja wa kitengo. Hii iliashiria wema au ubaya, mungu mwenyewe ndiye ajuaye.

Hii ilikuwa tarehe 7-9-2009 siku ya kukumbukwa. Kwani alichoniitia bosi ndio hicho nilichokuwa nikikiwaza siku kadhaa zilizopita. Nikiwa naelekea ofisi ya huyu bosi huku nawaza naitiwa nini kwani tangu waletwe jamaa toka la nywele za mahindi, mabadiliko mengi yamekuwa yakitokea. Kwa ujumla hawa jamaa wakifika mahala huwa wanakuja na sera zao, sio nawateta kwa ubaya, lakini kwa wale wanaowajua wataniunga mkono.

Hatua za kutoa kwenye kitengo changu kuelekea kwa bosi zilikuwa kama zile zinazoonyweshwa ndani ya sinema za mwendo wa kunyata, ingawaje nilikuwa natembea kawaida ila mwili ulikuwa siwangu tena. Utashangaa, kwani akili kwa upande mwingine iliwazaa matumaini na kwamba kama inawezekana nimwambie huyo bosi yaliyonikuta wikiend, manake jumamosi nilienda benki nikakuta laki tatu zangu zimechukuliwa kwa njia ya ATM, kwa miujuza, na cha ajabu watu wa benki waling'ang'ania kuwa huenda kuna mtu aliitumia ATM kadi yangu,ilihali kadi hiyo haibanduki mfukoni. Kwa hili nawashauri sana wateja wa ATM, kuhakikisha kila wanapochukua hela wawe wanaangalia salio kabla hawajaondoka ndani ya chumba cha ATM.

`I dont know how i am going to tell you this....' Alianza kwa Kiingereza chake cha Kimarekani, na baada ya bla-bla nyingi akapasua jipu na kusema `kitumbua chako kimisha kwenye kampuni hii, ikifika mwisho wa mwezi huu basi, ndio mwisho wamkataba wako na mwisho ajira wa kampuni hii'

Nilishindwa kuwaza, na mwili ulijiegeeza nyuma kiti,na taswira za watoto wakililia ada shule zilinijia, taswira na mzee wangu akilalamika hela ya matumizi, na taswira nyingi za ajabu zikawa zinacheza usoni...

Jamani hakuna kitu kinauma pale unapoambiwa kuwa kile kibarua kilichokuwa kikikuingizia vijisenti kimeota majani, na baya zaidi ikiwa kampuni zetu hizi zisizo na mikataba mizuri ya ajira inayomlinda mfanyakazi,ukimaliza mkataba basi unalipwa mshahara wa mwezi na hakuna kingine.

Wakati natoka mlangoni mwa bosi , simu ikaita, niliipokea nikiwa nimechanganyikiwa , nilitamani nimjibu ovyo aliyepiga, lakini niligundua ni sauti ya kaka yangu, na alichokuwa akinieleza sikuamini masikio yangu `Mdogo wako amefariki jana usiku...'

Ilikuwa jumatatu ngumu kwangu, nilipofika mezani nilikuta machozi yakija kwa kasi ,(mtu mzima akilia kuna jambo) nilikimbilia bafuni ambapo sikuweza kuvumilia, niliyamwaga machozi, na hatimaye nilimshukuru mungu. Nilikumbuka usemi usemao, mlango wa riziki mtoaji ni mungu na ukifungwa huko hufunguliwa kwingine. Na hujui ni ni kitakachofuata baadaye. Na kweli nilijipa moyo na kuaga kwenda msibani.

From miram3.com

1 comment :

Anonymous said...

Poleni sana wabongo, hilo ndilo mlilolitaka, nikiwaambia ni heri ya kuishi Ulaya mfungwa kuliko kuishi bongo raia mnanibishia mtakula jeuri yenu