Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, September 24, 2009

Hujafa Hujaumbika

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi ya tarehe 19-09-2009, nikiwa nasubiri daladala nifike Kariakoo,kuangalia kuwa sikukuu itaendaje.

Sikuamini niliyemuona mbele yangu kuwa alikuwa mmoja wa `Collage-mate wangu', nakumbuka kwa mara ya mwisho nilikutana naye akiwa ndani ya Benz lakifahari na my wife wake na kiti cha nyumaa cha hilo gari aliweka mbwa-mkubwa. Niliogopa hata kumsimamisha, siunajua tena ukikutana na wenzako unaowajua halafu ukajikuta wewe ni TZ 11, unajisuta mwenyewe. Lakini yote ni makadrio ya Mungu hamuwezi nyote mkawa sawa.

Nakumbuka tukiwa shuleni jamaa huyu alikuwa kati ya vijana watanashati, na pamoja na utanashati alikuwa nazo, na zaidi ya hapo ni mnato. Na hii ni hulka ya kibinadamu unapokuwa umejaliwa kipato, uzuri , au cheo mnato haubanduki, hata sauti hubadilika, utaongea kama mzungu hata kama kizungu hukijui, utaongea kama bosi hata kama hujawahi kushika nyazifa yoyote kwenye ofisi yoyote, hii ni hulka ya kibinadamu.

Mara lile gari likasimama mbele kidogo na niliposimama, nikajifanya sikuliona na kuangalia upande wa pili wa barabara, lakini haikusaidia kitu, kwani honi ya lili gari ilisikika, na mara nikasikia sauti yangu ikiitwa. Ilibidi nisijivunge, niligeuza kichwa na kuelekea pale gari liliposimama, huku moyoni wangu ukijisemea huenda hata kama sitapata lifti,lakini senti kidogo nitapatiwa, hii ni hulka yetu sie matawi ya chini, kuomba upate msaada kwa unayemuona anauwezo, kwasababu huna jinsi.

Nilichepuka hadi pale gari liliposimama,na mara kiyoo kikashushwa, na nilijikuta nikihema kwa woga, sio kwamba mimi ni mwoga, lakini lile jibwa, siunajua mijibwa mikubwa ilivyo, basi lilie likuwa miongoni mwa hiyo mijibwa. Lilikuwa limetulia kiti cha nyuma na macho yake yakiniangalia kwa hasira, na kusubiri nini bosi ataliamurisha.

`Usija-ali, rafiki yangu, vipi unaelekea wa-api, manake nampeleka wife kidogo shooping,na halafu...' alipofika hapo akaangalia nyuma ya gari, nikamuelewa ana maana gani.

`Usijali rafiki yangu, mimi nami namsubiri jamaa mmoja hapa, halafu nitaelekea huko ninakokwenda, usijali, hali zenu lakini' nilisema kwa hali ya kutojiamini kidogo

`Ok, basi chukua elifu kumi hii utachukua teksi , halafu, hii ni bussiness kadi yangu tutawasiliana' Alinipa business kadi yake wakati huo mai-wife wake alikuwa akiniangalia kwa dharau, na alimgusa begani mumewe kuonyesha kuwa wanachelewa.
Hii ilitokea takribani miaka mitano iliyopita, leo sura ninayoiona mbele yangu inafanana kabisa na yule rafiki yangu, lakini...

Nilimsogelea ili kuhakikisha, ni kweli ni yeye, pale alipo alikuwa kachoka kwakusimama,na mbaya zaidi alikuwa kashikilia fimbo iliyokuwa ikimsaidia kusimama, kuonyesha kuwa ana matatizo katika mguu au nyonga, chini kavaa ndala. Niliingiwa na simanzi kwasababu hata ndala alizovaa sio zile zakifahari kama ninavyomjua tabia yake. Jamani acheni Mungu aitwe Mungu, ina maana binadamu unaweza ukabadilika ghafla kutoka hali moja kuwa nyingine kiasi kwamba hata sura inabadilika kabisa.

`Ndio rafiki yangu usishangae sana, mimi ndio yule yule uliyemjua, ila mambo yamekwenda kidogo vibaya,lakini ninaimani kuwa baada ya siku kadhaa,mambo yatanyooka, siunajua tena fitina za watu, wameniharibia mipango yangu yote kiasi kwamba najuta hata kumwamini mtu. Wamefanya hata mke wangu kanikimbia..' alianza kuongea kama kaseti iliyofunguliwa.

Jamani nia kubwa hapa sio kumteta rafiki yangu,lengo kubwa ni kuonyesha hulka zetu wanadamu,ambazo wakati mwingine naweza kusema kuwa tunamkufuru mungu pale tunapojiona tunahali nzuri kikipato , kiuzuri kiwadhifa nk. Tunapenda kujisahau nakujiona tumefika. Hapana hatujafika kwasababu kabla hujafa hujaumbika, huwezi jua nini makadrio ya muumba,leo mzima keshomgonjwa taabani kitandani, lakini una miguvu, unatamba huko na huko,kesho unatembea mguu mmoja haupo. Yote hii ni kudura za muumba.

Tunatakiwa tukiwa katika hali nzuri au mbaya tumshukuru muumba kwani yote hayo hutokea kwa sababu, na sababu mojawapo ni ili tupate fundisho. Kama wewe unacho wakumbuke wasio nacho,watendee wema na punguza kunata,kwani huwezi jua huo mnato unaweza kugeuka kuwa mchatomchato. Kama wewe ni bosi, usiwadharau wafanyakazi wako, watendee haki, bila kujali mapungufu yao, kwani kila mmoja anayoridhiki yake kwako , ndio maana unapata unachopata. Na kama wewe huna kitu basi mshukuru mungu kwasababu huenda mwenyezi anakukwepesha ni mitihani kama hiyo inayowapata walicho nacho,huenda ungapata kama wao ungekufuru zaidi na hata kugeuka fisadi wa kutupwa.

Naomba niishie hapa,wakati natafakari aliyonisimulia huyu rafiki yangu, kwani mapaka sasa siamini kuwa ndio yule yule, ama kweli hujafa hujaumbika, naona hata hiyo riwaya tuipe hilo jina la `hujafa hujaumbika'.

Naombeni mawazo yenu washikaji ili nijue kama hiki ninachokiandika kinasaidia au kinabomoa

From miram3

No comments :