Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, August 20, 2009

MUJIBU WA SHERIA

Nimesikia kuwa enzi ya `mujibu wa sheria’ zinarudi tena, enzi hizo, ukibahatika kumaliza vidato au chuo ulitakiwa kulitumikia taifa kwa kwenda kwanza `kuhenya’ miezi sita na miezi sita ya mwisho kutoa huduma ndani ya JKT. Wengi waliobahatika wana hadithi nyingi kuhusiana na uwanja huu wa mujibu wa sheria.Nani anazikumbuka?
Narejea miaka ile ya 80’s mimi nilibahatika kutimiza sheria hii kule Mafinga na enzi hizo alikuwepo CO mmoja, mkali kwelikweli-Mlai. Huyu alikuwa akisimama smart-area akasema `heyii’ si kuruta, si green kwanja, kuku au..’ wote wanapotolea popote penye kujificha. Alikuwa akiogopewa kama jitu fulani kubwa, au kitu cha kutisha unachoweza kukifananisha nacho, hutaamini ukikutana naye, ni mfupi, mdogomdogo tu na mcheshi, lakini akiwa kazini popote pale yeye alikuwa kama simba aliyejeruhiwa. Walikuwepo afande `nusu-mungu’ alinyofolewa pete zake kwa ukali wake, yeye wakati anatukaribisha tuliambiwa kuwa yeye huanza kwa kusoma barua toka kwa mama yake ikimlalamikia kuwa awamu iliopita aliua kuruta wawili tu, hii imemvunja nguvu sana mama yake, na kama safari hii hataongeza mara kumi zaidi yake atamuachia laana.
Vituko vya JKT ni vingi na maelezo yake ni mengi na mengine huaanzia pale unapopewa taarifa kuwa unaenda kujiunga, wengi wanakuambia kuwa huko maji utayasikia kwenye bomba, kiasi kwamba chawa ni rafiki yako, wanajaa kwenye bukuta yako au kwenye `green vest yako ya njano’, na ili uwaue inabidi uiweke kwenye jiwe kubwa halafu uchukue jiwe jingine uanze kuwagonga-gonga,kwani ni wengi ajabu na ole wako uonekane ukiwaua, hairuhusiwi kwani ni sehemu yako, kuwaua ni makosa.
Nakumbuka siku tupo makao makuu ya JKT tunasubiri `bogi’ lakutupeleka kambini, tuliambiwa ukifika uwanja wa maeneo ya mafunzo, mizigo yako unatakiwa uruke nayo kichura, mfano kama umbali wa kutoka ulipopokelewa ni maili kadha basi wewe utaruka na mizigo yako, au utakimbia nayo hadi eneo lako la kufikia. Na mengi mengineyo, kama vile muda wa kula ni mchache na unapewa uji wamoto sana unawekewa kwenye `mistini’(bakuli au kikombe cha bati) na unatakiwa unywe kwa muda mfupi, dawa hapa ni kuongeza maji ili angalau kama utafanikiwa unywe kidogo.
Mimi nilipoingia mafinga kila kilichoelezewa nilikuta baadhi yake ni kinyume chake. Hutaamini, siku tuliyokaribishwa tulikaribishwa kwenye moto, kwani Mafinga kuna baridi ile mbaya, na kwa vile ilikuwa saa saba za usiku, tulilala pembeni ya huo moto hadi asubuhi. Na kesho yake tukasindikizwa na OC, hadi bwenini kwetu tukasajiliwa na kukabidhiwa kitanda. Muda wa kula ulikuwepo ila, mwanawane ilifika muda chakula unachopewa haushibi, hii sikudanganyi, na sio kuwa ni kichache, laa, huko kama unataka nitakusimulia baadaye. Kitanda tulipewa lakini kilikuwa kinaonekana kigeni, sababu gani niulize siku nyingine nitakuhadithia.
Ndugu zanguni, hakuna sehemu nzuri na yenye mafunzo ya ukakamavu kama JKT, ikirudishwa itapunguza mengi na nafikiri hata hawa vijana wanaovuta unga kama ingewezekana wakapelekwa huko, kwani baada ya muda wa mafunzo kuisha kama ni mwaka, au miezi sita,adabu na nidhamu ni asilimia mia.
Wale waliobahatika wenye hizi kumbukumbu naomba mziwakilishe ili ziwavutie kizazi cha sasa,ili na wao waone umuhimu wake.

From miram3.com

5 comments :

Anonymous said...

Umenikumbusha mbali wanawane, naomba lirejeshwe tena ili vijana wakomae

emuthree said...

Nashukukuru kwa kuunga mkono hoja hii.

Anonymous said...

Huwezi kujua uzuri wa jeshi mpaka upitie. Mimi mwenyewe nilikuwa 'selule' lakini jeshi lilinifundisha ukakamavu. Mwanamume unatakiwa uwe na uwe mgumu - uwe na uweza wa kupitia maisha magumu bila ya kusambaratika (uvumilivu).

Uzuri mwingine wa jeshi ni kwamba wote mnakuwa sawa, na pia unajifunza kutoka kwa watu ambao msingekutana ufz. Ukitoka jeshini wale mliokuwa nao jeshini mnakuwa na strong bond.
Kitu kingine unajifunza ni jinsi ya kutumia muda. Katika siku moja mtu unaweza kufanya mambo mengi sana.

Kama ningekuwa na uwezo ningelipia watoto wangu (wa kiume) waende jeshini wakifika umri.

Ila kwa experience yangu (Chita - 91-92) sikufurahia jinsi baadhi ya dada zetu (sio wote) walivyonyanyasika. Kwa wale waliopenda vya urahisi, au waliokuwa na udhaifu (pumu, au magonjwa mengine) baadhi ya maafande walitumia mwanya huo vibaya. Mmoja alikuwa anaumwa pumu, na wangemuua, kama ndugu yake asingemtorosha.

Ninaamini kuwa hii kasoro haikutokana sheria za JKT yenyewe bali kasoro na "abuses" za wale maafande tuliokuwa nao.

Ntibadyuza

emuthree said...

Nashukuru kuwa u mmoja wa waliofaidi dhamira ya baba wa taifa ya kujenga taifa la vijana au raia wakakamavu, na kuondoa tofauiti kati ya walionacho na wasionacho. Kama ulivyoona, wote ndani ya jeshi tulikuwa kitu kimoja, hakuna wa tajiri au masikini, kunyakua ni kunyakua, kuvaa greevest ya njano ni wote hivyohivyo...!
Nashangaa watu wanamuenzi wakati mambo yake kama haya wameyapiga buti, unajua kwanini, mtoto wa tajiri aende kuhenya, mtu nyanya...mmh, haya mngelijua siri ya jeshi nafikiri watoto waote wangepitia huko, leo hii kusingekuwa na wavuta unga!
Ahsante Ntibadyuza, nashukuru kwa kupitia hapa na kuacha ujumbe huu adimu, karibu sana

Anonymous said...

Vijana wa machips na maziwa ya makopo hawawezi kukumbuka enzi hiyo. JKT ilikuwa sehemu ya kujenga usawa, siku hizi hata maofisini utaona, kuna watoto wa wakubwa mishahara juu, na utawaona walivyo laini...tunamshukuru sana baba wa taifa kwa hili!