Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, July 14, 2009

MAMBO YA MAISHA





Maisha ni mlolongo wa mambo mengi, ambayo kila ukipita hili unakutana na lile, ni kamaduara linalozunguka,ni kama dunia yetu inavyozunguka, katiak mzunguko huo tunapata usiku na mchana. Na kila usiku au mchana wake kuna matukio yanatokea, sasakama hakuna kumbukumbu(diary) za kuhifadhi hayo matukio, utajikuta kila mara mgeni wa hili au lile.

Pia kuna mambo mengi mazuri yanayotokea katika dunia hii, matukio ya kila namna, na matukio hayo hayatokei tu, lazima kuna sababu, na hizo sababu zinaweza kuwa funzo kwetu, je tutakujae kuyajua hayo kama hakuna namna ya kuhifadhi hayo mambo, ....


 Katika kulifikiria hili nikaona nianzishe blog hii ili niweze kuweka kumbukumbu za matukio niliyokutana nayo au uliokutana nayo wewe.Kwa namna hiyo, ina maana kuwa, sitaweza kuweka kila kitu mwenyewe, wewe na yule mtakuwa wadau wazuri wa kuniwakilishia kile kilichokukuta maishani mwako.

Unaweza ukaelezea maisha yako ya ujana, shuleni au kazini au hapo unapoishi ili wengine wajue, wajifunze na watoe ushauri. Unaweza ukatuma kisa chako kwa mtandao, batua pepe,hata kwa simu na mimi nitaiweka mfano wa kisa,.

Kwa namna hii basi naomba tusiwe wachoyo katika kuchangia hili au lile.

AhsanteMiram3
Enhanced by Zemanta

2 comments :

Anonymous said...

Tatizo ndugu yangu ni muda, hata hivyo naweza nikajipinda kutenegeneza mambo kimaelezo, natuma kwenu mnaogopa kuiweka hewani. Na kama nikikutumia usipoiweka naomba unirudishie stori yangu!

emuthree said...

Huyu alikuwa mtu wa kwanza kuniwakilishia kisa chake, najaribu kukitafuta kilikwa kisa gani, ....je wewe una kisa chochote. hebu kilete, tukiweke hewani!